KUWA WA KWANZA KUSIKILIZA WIMBO MPYA KABISA WA MASHAUZI CLASSIC …ni Asia Mzinga na kitu “Ubaya Haulipizwi”




KUWA WA KWANZA KUSIKILIZA WIMBO MPYA KABISA WA MASHAUZI CLASSIC …ni Asia Mzinga na kitu "Ubaya Haulipizwi"
KUWA WA KWANZA KUSIKILIZA WIMBO MPYA KABISA WA MASHAUZI            CLASSIC …ni Asia Mzinga na kitu

HAKIKA maji yanafuata mkondo. Huyu ni Asia Mzinga (pichani juu) binti wa mwimbaji mkongwe wa taarab Bi Mwanamtama Amir. Hapa ameshuka na bonge la wimbo.

Baba mzazi wa Asia Mzinga anayekwenda kwa jina Hamis Mzinga nae pia ni mwimbaji na mtunzi maarufu wa muziki wa taarab akiwa amepata kutamba na kundi la Egyptian. Moja ya wimbo uliotamba sana wa Hamis Mzinga ambaye kwa sasa anaishi Uingereza ni "Mazao Bora shambani".

Kwa Asia Mzinga hii inakuwa ni mara yake ya kwanza katika historia yake ya kimuziki  kurekodi wimbo wa taarab. Mwenyewe ameiambia Saluti5 kuwa shukran za dhati zimwendee Isha Mashauzi kwa kumfungulia ukurasa mpya kwenye maisha yake.

Wimbo huu umepewa jina la "Ubaya Haulipizwi" utunzi wake Isha Mashauzi. Wengi waliokuwa wakiusikia ukumbini wimbo huu waliuzoea kwa jina la Wema Hauozi lakini jina halisi la wimbo ni Ubaya Haulipizwi.

Umerekodiwa katika studio za Soft Records chini ya producer Pitshou Mechat Shemesha ambaye pia ndiye aliyekung'uta mpini wa solo gitaa.

Kinanda kimepigwa na Kali Kitimoto wakati bass limepigwa na Jumanne Mussa (J Four - Jonh Cena).

Ni wimbo mtamu wa dakika 8 wenye ujumbe mzuri ndani yake ambao unatosha kuwa jibu tosha kwa wale wote wanaoipiga madongo Mashauzi Classic. Ni majibu ya kistaarab yanayoashiria kuwa watu wanataka kufanya kazi na hawana muda wa malumbano.

Saluti5 ndiyo nyumba ya muziki wa dansi na taarab, ngoma zote mpya zinadondoka hapa kwanza kabla ya kusambaa sehemu zingine. Usikilize wimbo huu hapo chini.



Comments