KIPIGO CHA GOLI 5-3 ILICHOAMBULIA MANCHESTER UNITED SIRI YAFICHUKA


KIPIGO CHA GOLI 5-3 ILICHOAMBULIA MANCHESTER UNITED SIRI YAFICHUKA
Siri ya kipigo kizito ilichokipata klabu ya Manchester United kutoka kwa klabu iliyopanda daraja msimu huu ya Leicester City imefichuka.
Taarifa zilizozagaa nchini Uingereza zinadai kuwa wachezaji na viongozi wa klabu ya Leicester City walifanyiwa maombi maalumu kutoka kwa mmoja kati ya viongozi wa dini ya Kibudha waliokuwepo uwanjani King Power Stadium kwaajili ya kazi hiyo maalumu. 
Wachezaji wa timu hiyo walifanyiwa maombi maalumu na kupewa mikono ya baraka ambayo inaaminika ndio iliyowasaidia kuupata ushindi huo wa kihistoria dhidi ya Manchester United kutoka kwa makasisi hao wa dini ya Kibudha waliofanya kazi hiyo kwenye dimba la King Power Stadium.



Taarifa zinadai kuwa wafungaji wa magoli ya Leicester City David Nugent na Jamie Vardy walivalishwa mavazi maalumu ya Kibudha mara baada ya ushindi huo wa jumla ya magoli 5-3 wakati meneja wa timu hiyo Nigel Pearson alishindwa kuzizuia hisia zake mara baada ya mcheazo huo pale alipokwenda kuwakumbatia viongozi hao wa kidini ikiwa ni ishara ya kutoa shukrani kwao kwa kuwa sehemu ya ushindi huo na kuwaambia kuwa wanakaribishwa uwanjani hapo kila mara timu hiyo itakapokuwa inacheza ili waweze kufanya maombi hayo.
Mmiliki wa klabu hiyo ambaye ni raia wa Thailand Vichai Srivaddhanaprabha alisafiri na viongozi hao wa kidini kutokea mashariki ya mbali na mara alipofika nao nchini Uingereza walikwenda kwenye kiwanja cha mazoezi cha timu hiyo na mara moja maombi maalumu yakaanza kwaajili ya mchezo huo dhidi ya Manchester United.
Wiki moja kabla ya msimu kuanza mahema maalumu yalifungwa kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo na viongozi hao wa kidini wakafanya maombi maalumu kwa viongozi na wachezaji wa timu hiyo yenye malengo ya kuwapa baraka ambapo inasadikika kuwa maombi hayo yameisaidia sana timu hiyo kuto kupoteza mchezo wowote ule wa nyumbani dhidi ya vilabu vya Everton, Arsenal na hatimaye Manchester United.
Mara baada ya kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi daraja la kwanza nchini Uingereza (Championship) wachezaji na viongozi wa timu hiyo walizuru kwenye eneo la Phra Maha Mondop mahali ambapo majumba ya ibada za Kibudha kwenye mji wa Bangkok yalipo kwaajili ya kutoa shukrani kwa maombi waliyofanyiwa mpaka wakaweza kuwa mabingwa na hatimaye kupanda daraja.


Comments