Je,Unamfahamu Sensei Magoma Nyamuko Sarya??


Je,Unamfahamu Sensei Magoma Nyamuko Sarya??
Sensei Magoma N. Sarya ndiye aliyekuwa gwiji wa Karate na kiungo muhimu kwa sensei N. C. Bomani katika kuendeleza mwenendo wa Sanaa ya Karate nchini Tanzania. Sensei Magoma (Daud) amefundisha wanafunzi wengi wa Karate nchini Tanzania Zaidi ya mwalimu yeyote hapa nchini. 

Amekuwa mwafunzi kiongozi mwenye mamlaka ya kusimamia Zanaki dojo na matawi yake Tanzania tokea mwaka 1976 hadi 1982.

Sensei Magoma ni mmoja kati ya wanafunzi wa tano nchini kupata shahada ya kwanza "Shodan" mkanda mweusi mwaka 1976 akiwa mwenye umri mdogo kulikoni wenzake wote chini ya sensei Bomani. Wanafunzi hao ni: Sensei Mapfumo Gamanya ( Mzibabwe), sensei Tola Sodoinde Malunga, Sensei Abome Mabruki na kaka yake sensei Adombe Mabruki, na mwisho kwa umri kati ya hao ni Sensei Magoma Nyamuko Sarya.


Wakati sensei Bomani akiwa nje ya nchi huko nchini Marekani kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1981 sensei Magoma ndiye alikuwa mwanafunzi mkuu kiongozi na mwenye mamlaka yote ya mapendekezo na kutoa test na hata mikanda yote ya mtindo wa Okinawa Goju Ryu Kyokai chini ya mfumo wa kiongozi wao wa Karate duniani Master Eiichi Miyazato, mwalimu wa sensei Bomani. Vigumu mno kuwataja wanafunzi wote waliopitia chini yake, bali tu, kila mwanafunzi aliyekuwa dojo kwa miaka ya 1976 hadi 1982 alikuwa chini ya himaya yake.


Licha ya kuwa mkufunzi mkuu wa Karate nchini Tanzania, mara tu baada yakuondoka kwake mwaka 1982 hapa nchini kuelekea nchi za mashariki ya mbali ikiwemo, India, Nepal, Singapore, Malaysia na Phillipines. Mwalimu Magoma aliacha pengo kubwa ambalo hadi hii leo hamna hata mwenye kuweza liziba katika kuimarisha Sanaa ya Karate Tanzania.

Sensei Magoma pia, ni mkufunzi wa Sanaa ya Yoga na anauzoefu mkubwa katika fani hiyo ambayo ilimpeleka nchi nyingi akiwa kama mwalimu na wakati huohuo kufundisha Karate. Alipata mafunzo ya Sanaa ya Yoga nchini India kutoka katika chuo cha "Neo- Humanist Studies" katika mji wa Varanasi, mwaka 1983.


Mengi aliyoyafanya akiwa bado yupo nchini kwa wakati huo, ni pamoja na kutenganisha darasa la mafunzo ya Karate la watoto na watu wazima na kuliita kwa jina ka heshima ya mwanzilishi wa shule hiyo " Bomani Brigade" au "BB" kama ilivyokuwa anaitwa.


Kundi hilo la vijana wagodo, lilikuwa halisomi Karate tu, bali pia mwalimu Magoma alijitolea muda wake wote kuwasaidia kimasomo yao kama vile kuwafundisha "Tuition" ya hisabati, Kiingereza, na kuandika isha mbalimbali zinazohusu maisha kiujumla. Leo hii, ni Zaidi ya miaka takriban therasini na wale vijana wamefaidika sana kwa mfano kuna wengi wao kwa hivi sasa ni walimu wa Sanaa ya Karate pia.

Sensei Magoma, ni mwalimu mwenye upeo wa hali ya juu sana katika Sanaa ya Karate ya Okinawa Goju Ryu Karate-do Jundokan Kyokai na kama nilivyoeleza hapo awali, ameacha pengo kubwa mno ambalo sasa ni dhahiri kwamba kurejea kwake katika kufundisha sanaa hii nchini, kunaweza kuwahamasisha walimu wengi na kuiga mfano wake wa kuwa na moyo na nia ya kusaidia vijana na kuwapa nishani katika maisha yao ya baadae.

Kwa mengine Zaidi yanayohusika na Sensei Magoma na jinsi yakuwasiliana nae yatafuatia hao baadae.


Comments