BEKI wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher ameonyesha kuduwazwa kwake na usajili wa Manchester United uliotumia pesa nyingi lakini ukishindwa kumnunua beki wa kiwango cha juu.
Akiongea na Sky Sports kuhusu mechi ya United ya kipigo cha 5-3 kutoka kwa Leicester City, Jamie Carragher alishutumu maamuzi ya refarii Clattenburg yaliyochangia penalti tata lakini akasema usajili wa United unaonyesha udhaifu mkubwa wa kiutawala.
"Kutumia pauni milioni 150 kwenye usajili bila kupata saini ya beki wa hali ya juu, ni jambo la kushangaza," alisema Carragher.
Comments
Post a Comment