ILIKUWA NI KARAMU YA PENALTI! LIVERPOOL YAVUKA KWA MATUTA 14 -13 …kinda wa Liverpool Jordan Rossiter usipime
KAMA penalti zina raha basi Jumanne usiku mashabiki wa soka walistarehe. Mechi ya Capital One ya Liverpool na Middlesbrough ikaamuliwa kwa matuta 30 – wachezaji wote wakapiga penalti hadi wengine wakarudia.
Mechi iliyochezwa kwa dakika 120, iliisha kwa sare ya 2-2 na ndipo ukawadia wasaa wa matuta, kila timu ikapiga mikwaju 15, Liverpool ikipoteza moja na Middlesbrough ikakosa mbili.
Kinda wa Liverpool Jordan Rossiter mwenye umri wa miaka 17, alitakata na kuifanyia kweli mechi yake ya kwanza kwa kutupia wavuni bao la kuongoza dakika ya 17 kabla Adam Reach hajasawazisha dakika ya 63.
Suso akaifanya Liverpool iwe mbele dakika ya 109 lakini Patrick Bamford akaisawazishia Middlesbrough ilipotimu dakika ya 120. Tazama chati hapo chini kuona namna penalti zilivyopigwa.
LIVERPOOL (4-2-3-1): Mignolet 6: Manquillo 6, Toure 6.5, Sakho 5, Enrique 6: Rossiter 7 (Williams 79mins), Lucas 6: Sterling 7, Lallana 6, Markovic 5: Lambert 6 (Balotelli 74mins)
MIDDLESBROUGH (4-4-2): Blackman 6: Fredericks 7, Ayala 7, Omeru 6.5, Friend 7: Adomah 7, Clayton 7.5, Leadbitter 8.5, Reach 7.5: Tomlin 8, Kike 7 (Wildschut 76mins).
Comments
Post a Comment