HAYA NDIO MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LIGI KUU YA ENGLAND ZILIZOCHEZWA JUMAMOSI …Lampard aendelea kuibeba Man City
TIMU 16 za Ligi Kuu ya England zilijitosa viwanjani jana Jumamosi kusaka pointi tatu muhimu na kushuhudia Liverpool na Arsenal zikibanwa kwa sare huku wapinzani wao wakubwa wakiibuka na ushindi.
Manchester City, Chelsea na Manchester United zikaibuka na ushindi. Timu hizi tatu pamoja na Liverpool na Arsenal ndizo zinazotarajiwa kuwa na vita vikuwa vya kuwania nafasi nne za juu (Top 4)
Hadi dakika ya 21, Machester City iliyokuwa ikiumana na Hull City iliongoza 2-0 kwa magoli ya Sergio Aguero na Edin Dzeko lakini wakashuhudia beki wao mpya Eliaquim Mangala akijifunga kabla Abel Hernandez hajafunga kwa penalti na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa 2-2.
Edin Dzeko akafunga la tatu dakika ya 68 huku kiungo mkongwe Frank Lampard akihitimisha ushidi kwa bao la dakika ya 87.
Haya ndio matokeo kamili ya mechi zote za Jumamosi.
Liverpool 1 - 1 Everton
Chelsea 3 - 0 Aston Villa
Crystal Palace2 - 0Leicester
Hull 2 - 4 Man City
Man Utd 2 - 1 West Ham
Southampton 2 - 1QPR
Sunderland 0 - 0 Swansea
Arsenal 1 - 1 Tottenham
Comments
Post a Comment