HATIMAYE MUUMIN APANDA JUKWAA LA G5 MODERN TAARAB KWA MARA YA KWANZA …aimba live wimbo wake wa Kigodoro

MWINJUMA Muumin ambaye anajulikana zaidi kwa umahiri wake wa kwenye muziki wa dansi, Jumamosi usiku kwa mara ya kwanza aliimba live wimbo wake wa taarab.

Japokuwa Muumin ameshawahi kutumbuiza mara chache mikoani kwa kutumia wimbo wake huo unaokwenda kwa jina la "Kigodoro" lakini Jumamosi alikuwa anatumbuiza kwa mara ya kwanza akiwa na bendi rasmi iliyorekodi wimbo huo – G Five Modern Taarab.

Hiyo ilikuwa ni katika ukumbi wa Flamingo Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam ambako kundi hilo linapatikana katika kila siku za Jumamosi.

Muumin alishangiliwa sana na hata aliposhuka jukwaani mashabiki kadhaa walimfuata na kumzunguka.

Mkurugenzi wa G Five, Hamis Slim ameiambia Saluti5 kuwa Muumin ni mwanachama wao na hivyo kila atakapokuwepo jijini Dar es Salaam basi atakuwa akipanda jukwaa lao.

Comments