HATIMAYE FM ACADEMIA WAINGIZA SOKONI AUDI CD NA DVD ZA ALBAM YA CHUKI YA NINI



HATIMAYE FM ACADEMIA WAINGIZA SOKONI AUDI CD NA DVD ZA ALBAM YA CHUKI YA NINI
HATIMAYE FM ACADEMIA WAINGIZA SOKONI AUDI CD NA DVD ZA            ALBAM YA CHUKI YA NINI

BAADA ya kusubiri kwa zaidi ya nusu mwaka, hatimaye mashabiki wa FM Academia "Wazee wa Ngwasuma", sasa wanaweza kununua Audio CD na DVD za albam ya "Chuki ya Nini"

Albam hiyo iliyozinduliwa mwishoni mwa mwaka jana pale Mzalendo Pub jijini Dar es Salaam, ilishindwa kuingia sokoni baada ya bendi hiyo kuamua kwenda kuchapa nakala za "Chuki ya Nini" nje ya nchi ili kulinda ubora wa kazi yao.

Saluti5 imeshuhudia albam hiyo ikiuzwa na wahusika wa bendi hiyo katika maeneo kadhaa ya jiji.

Rais wa FM Academia Nyoshi el Saadat hivi karibuni aliiambia Saluti5 kuwa watafanya onyesho kubwa la kufungua rasmi mauzo ya albam yao ya "Chuki ya Nini".

Albam hiyo inaundwa na nyimbo sita: "Chuki ya Nini", "Fataki", "Otilia", "Ndoa ya Kisasa", "Neema"  na "Dai Chako Ulaumiwe".

Pichani juu ni namba Audio CD na DVD za "Chuki ya Nini" zinavyoonekana kwa nje.



Comments