FRANK LAMPARD MWIBA MCHUNGU KWA CHELSEA …AISAWAZISHIA MAN CITY DAKIKA ZA LALA SALAMA …Diego Costa atoka mtupu
KWA mara ya kwanza tangu aanze kuichezea Chelsea katika mechi za Ligi Kuu ya England, mshambuliaji Diego Costa ametoka bila kufunga kwenye mchezo dhidi ya Manchester City.
Kama vile hiyo haikutosha, kiungo za wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard aliyeingia dakika ya 78 akawa mwiba mkali kwa timu yake ya zamani baada ya kuisawazishia City bao.
Ulikuwa mchezo mkali uliokamilika kwa sare ya 1-1 huku City wakicheza pungufu kuanzia dakika ya 66 baada ya beki Pablo Zabaleta kulambwa kadi nyekundu.
Chelsea walipata bao lao katika dakika ya 71 kupitia kwa mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Andre Schuerrle, lakini Lampard anayeichezea City kwa mkopo akachomoa dakika ya 88.
Kabla ya mchezo huu, Chelsea ilikuwa imeshinda mechi zake zote nne huku Costa akicheka na wavu katika kila mchezo na kujikusanyia jumla ya mabao 7.
Comments
Post a Comment