KIONGOZI wa Five Stars Modern Taarab 'Watoto wa Bongo', Ally Juma 'Ally J', Oktoba 6, mwaka huu, anatarajia kukiingiza kambini kikosi chake kwa ajili ya maandalizi ya albamu yao ijayo, imefahamika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ally J alisema kuwa, wamekuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na tatizo la ukosefu wa vyombo ambapo hivi sasa kila kitu kiko sawa.
Ally J alisema, maandalizi ya albamu yao hiyo mpya yatakwenda sambamba na usajili wa wasanii wanaokuja kuongeza nguvu kwenye kundi hilo, ambao wengi wao ni chipukizi lakini wenye uwezo mzuri jukwaani.
"Albamu yetu mpya itakusanya vibao sita ambavyo baadhi yake ni 'Kichambo Kinakuhusu', 'Doa la Ubaya', 'Big Up My Dear', 'Penzi si Hatia', 'Sina Gubu Nina Sababu'," alisema Ally J.
Aliwataja badhi ya wakongwe atakaoingia nao kambini kwenye ukumbi wa Chinese, Temeke Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam, kuwa ni pamoja na waimbaji Zena Mohammed, Mwamvita Shaibu, Mussa Kijoti na Mariam BSS.
Comments
Post a Comment