DOGO MFAUME ASEMA AMEACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA



DOGO MFAUME ASEMA AMEACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

DSCN8501'NIMEACHA madawa ya kulevya', hayo ndio maneno aliyosema Dogo Mfaume siku ya Jumamosi tarehe 20, wakati wadau mbalimbali wa sanaa na burudani, , walipo  DSCN8503    jitokeza kwa wingi kwenye onesho maalum la harambee ya kumchangia mama yake Dogo Mfaume, Flora Shayo aliyekatwa miguu kwa maradhi ya kisukari.

Onesho hilo lililoanza kuunguruma majira ya saa 3:30 usiku na kuendelea hadi majogoo, lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii kibao wa miondoko tofauti ya muziki.

Licha ya pesa nyingi alizochangiwa bi Flora, bado wadau kemkemu walimwaga ahadi za kutoa misaada kwa mama huyo, ili kumwezesha kuishi kwa unafuu zaidi wa maisha.

Badhi ya misada mingine aliyoahidiwa bi Flora ni pamoja na baiskeli ya magurudumu manne, magongo ya mazoezi pamoja na bajaj kwa ajili ya DSCN8518kumpatia pesa za kumsaidia kwa chakula.

Wakati huohuo, msanii wa miondoko ya Mchiriku, Mfaume Makuka 'Dogo Mfaume' ameuhakikishia umma wa mashabiki wa burudani, kuwa hivi sasa ameachana kabisa na utumiaji wa madawa haramu ya kulevya.

Tukio hilo la Mfaume kuudhihirishia umma wa mashabiki suala hilo, lilitokea Jumamosi, kwenye ukumbi wa Sandiego, Tandika, jijini Dar es Salaam, kwenye onesho maalum la harambee ya kumchangia mama yake, Flora Shayo.

Harambee ya kumchangia bi Flora iliandaliwa na Viumbe Wazito Promotion, ili kumsaidia mama huyo aliyekatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi ya kisukari yanayomsumbua hadi sasa.

"Ni kweli nilikuwa natumia madawa ya kulevya, lakini hivi sasa nimeachana nayDSCN8535o kabisa, kwani rafiki zangu walikuwa wananitenga, pia mama yangu nilikuwa nikimtia simanzi kwa kitendo hicho," alisema Mfaume.

Mfaume alisema kuwa, kuna athari nyingi zilizomtokea, kama vile; kutojishughulisha kutafuta riziki na kumsababishia maisha yake kurudi nyuma kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake, bi Flora alisema kuwa anafurahi kusikia kuwa mwanawe ameacha kujihusisha na ulevi huo wenye madhara makubwa kwa mtumiaji na familia yake, ambapo sasa ameahidi kuzidi kumpenda na kuwa naye karibu zaidi.DSCN8520DSCN8519



Comments