DANSA MASTER B ALIYETOKEA EXTRA BONGO AITOSA TWANGA NA KUIBUKIA MASHUJAA BAND …hii ni mara yake ya pili kuifanyia kitu mbaya Twanga
DANSA mkali kwa free style Master B (Pichani juu) ameipiga chenga ya mwili Twanga Pepeta na kuibukia Mashujaa Band.
Master B alijiunga na Twanga siku chache zilizopita akitokea Extra Bongo na akashiriki maonyesho kadhaa Twanga Pepeta lakini akageuza kibao na kujiunga na Mashujaa Band ambapo kuanzia Ijumaa iliyopita alianza kuitumika rasmi ofisi yake mpya.
Hii si mara ya kwanza Master B kufanya hivyo kwa Twanga. Mwaka jana aliikacha Extra Bongo na kujiunga na Twanga Pepeta lakini baada ya wiki chache akaenda 'kumpigia magoti' Chocky na kurejea Extra Bongo.
Twanga wakiamini kuwa dansa huyo wa kiume sasa katulia, wakajikuta wanakutana na hadithi ile ile, jamaa kateleza hadi Mashujaa Band.
Comments
Post a Comment