CHOCKY AWATAKIA KILA LA KHERI KINA BANZA STONE


CHOCKY AWATAKIA KILA LA KHERI KINA BANZA STONE
CHOCKY AWATAKIA KILA LA KHERI KINA BANZA STONE

LICHA ya Banza Stone na wenzake waliojiengua Extra Bongo na kuibuka na maneno ya kejeli, lakini bosi wao wa zamani - Ally Chocky amesema anawatakia kila la kheri.

Banza Stone, Athanas Montanabe, Adamu Bombole, Adam Hassan na wengine kadhaa, wamejiengua Extra Bongo na kuanzisha bendi mpya WANA EXTRA.

Bendi hiyo ikafanya onyesho lake la kwanza Jumapili iliyopita pale Flamingo Bar Magomeni Mwembechai ambapo Banza Stone akasema wao ni wafungwa waliotoroka jela ya mateso.

Kuonyesha msisitizo Banza na Athanas wakasema wanajilinganisha na ile filamu marufu ya Escape from Sobibor iliyojaa matukio ya ukatili kambini.

Lakini Chocky alipoongea na Saluti5 jana jioni akasema anashukuru kwa kauli hizo ambazo alidai pengine ndio sehemu ya uungwana wa wasanii hao.

"Nawatakia kila la kheri, tunaamini siku zote msanii anapenda sehemu yenye maslahi na itakayompa utulivu wa namfsi, labda hiyo ni sehemu sahihi kwao, sina la cha kuongeza zaidi ya kuwatakia kila la kheri.

"Kama wameruka majivu na kukanyaga moto au wameruka moto na kukanyaga majivu basi itajulikana hapo baadae," alisema Ally Chocky.

Kwa mtu aliyehushudia maonyesho yote mawili Jumapili iliyopita (Extra Bongo – Garden Breeze na Wana Extra – Flamingo Bar), atakuwa shahidi kuwa kiutendaji wa jukwaani hakuna pengo lililoonekana Extra Bongo.

Badala ya kupwaya kwa kiwango cha utumbuizaji jukwaani, ndio kwanza Extra Bongo ikapiga kazi iliyokwenda shule – burudani iliyoonea kila idara -uimbaji mzuri, upigaji mzuri. Utoto utoto hakuna.

Katika onyesho hilo la Extra Bongo, Chocky akawa mjanja zaidi kwa kutumbuiza kama vile hakuna kitu kinachoitwa Wana Extra, hakuizungumzia hata kwa sekunde moja. 



Comments