CHELSEA YAENDELEA KUGAWA DOZI YA RAHA KWA MASHABIKI WAKE …Diego Costa wembe ule ule




CHELSEA YAENDELEA KUGAWA DOZI YA RAHA KWA MASHABIKI WAKE …Diego Costa wembe ule ule

Chelsea striker burst into life with a crashing                    header on the hour and was the catalyst for another in                    his side's comfortable victory at Stamford Bridge

CHELSEA imeendelea kujitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Aston Villa 3-0 .

Villa ambao waliwashangaza watu wengi kwa namna walivyoanza ligi kwa kishindo na  kujizolea pointi 10 katika mechi zao tano za mwanzo, ilianza kwa kuibana Chelsea lakini ikajikuta ikifungwa bao la mapema.

Baada ya kushuhudia shuti lake likiokolewa, Willian aliyekuwa akicheza upande wa kulia, akamtengea mpira Oscar ambaye bila ajizi akafunga bao la kwanza katika dakika ya 7.

Vijana wa Jose Mourinho wakaandika bao la pili ilipotimu dakika ya 60. Beki wa kushoto Cesar Azpilicueta akamchongea krosi safi Diego Costa aliyefunga kwa kichwa.

Willian ambaye alihusika na magoli yote mawili akafunga bao la tatu dakika ya 79.

CHELSEA 4-2-3-1: Courtois 6.5; Ivanovic 7, Cahill 5.5, Terry 6, Azpilicueta 6; Fabregas 7, Matic 7; Willian 7.5, Oscar 7 (Mikel 77), Hazard 6 (Schurrle 68, 6); Costa 7 (Remy 81).

ASTON VILLA 4-5-1: Guzan 6.5; Hutton 6, Senderos 6, Baker 6, Cissokho 6; Richardson 6 (Bent 69, 5), Cleverley 6.5, Westwood 6.5, Delph 7, Weimann 5 (N'Zogbia 69, 5); Agbolahor 7.



Comments