BRENDAN Rodgers amempongeza Mario Balotelli kwa utulivu aliouonyesha kwenye mechi dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Everton.
Balotelli ambaye bado hajaifungia bao lolote Liverpool kwenye Barclays Premier League, alipoteza nafasi kadhaa za kudumbukiza mipira wavuni.
Angeweza kufanya matokeo yasomeke 2-0 muda mfupi baada ya Steven Gerrard kufunga bao la kuongoza, lakini shuti lake la karibu likagonga mwamba. Baadae Phil Jagielka akaisawazishia Everton na kufanya mchezo ukamilike kwa sare ya 1-1.
Mshambuliaji huyo wa Italia alifanyiwa rafu kadhaa lakini akawa mpole na kuwekeza zaidi akili yake kwenye mchezo.
Rodgers alisema: "Anapaswa kuzingatia mchezo na nilimwelekeza hilo kabla ya mchezo. Hii ni mechi ambayo huibua hisia kali na inaweza kumwia vigumu mchezaji."
Baada ya mchezo, Balotelli alipigwa picha akikataa mitaa ya Merseyside huku akionekana yuko poa na mwingi wa amani.
Comments
Post a Comment