BENDI VICTORIA SOUND KUZINDULIWA RASMI OKTOBA 4 NEW MSASANI CLUB …Malaika Band kusindikiza

BENDI ya Victoria Sound iliyotesa na wimbo "Shamba la Bibi" chini Mwinjuma Muumin kabla ya kufa kifo cha kawaida, itatambulishwa rasmi tarehe nne mwezi Oktoba baada ya kusukwa upya.

Victoria Sound ambayo itakuwa bendi ndugu na Malaika Band, inaundwa na wanamuziki kadhaa kutoka Msondo Ngoma na Sikinde, wakiwemo mpuliza saxophone Shaaban Lendi Edo Sanga,  Adolph Mbinga, James Mawila na Karama Legesu.

Msemaji wa bendi hiyo Promota Bonga, ameiambia Saluti5 kuwa New Victoria Sound itatambulishwa ndani ya ukumbi wa New Msasani Club huku wakisindikizwa na Malaika Band

Naye Karama Legesu ameimbia Saluti5 kuwa bendi yao tayari imerekodi nyimbo tatu kwa njia ya audio na video na muda mfupi zitabisha hodi kwenye vituo vya radio na televisheni.

Amezitaja nyimbo hizo kuwa ni "Tazama Mbele" uliotungwa na Edo Sanga, "Uonevu" utunzi wake yeye mwenyewe (Karama Legesu) na "Mpenzi Jojoo" uliotungwa na kiongozi wa bendi Janas Nembuka.

Comments