AUDIO: MSIKILIZE CHOKORAA ALIVYOICHINJIA BAHARINI TWANGA PEPETA …aikana safari ya kurejea African Stars Band

MWIMBAJI na mmoja wa wakurugenzi wa Mapacha Watatu, Khalid Chokoraa (pichani kushoto) amekanusha uvumi uliosambaa kuwa anarejea African Stars Band "Twanga Pepeta".

Akiongea na Saluti5 Jumapili usiku, Chokoraa alikiri kuwepo kwa uvumi huo lakini akawatoa hofu mashabiki wa Mapacha na kuwaahidi kuwa hana mpango wa kuiacha Mapacha Watatu.

Huku akiwa sambamba na meneja wa Mapacha Watatu, Khamis Dacota (kulia pichani), Chokoraa akasema kwa namna milango ya rizki inavyofunguka kwenye bendi yao, itakuwa ni jambo la ajabu yeye kuikimbia Mapacha.

Saluti5 imekuwa shuhuda wa tetesi hizo ambazo zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku mpaka kufikia hatua ya baadhi ya wadau muhimu wa Twanga kuthibitisha kuwa ni kweli mipango ya kumrejesha Chokoraa ipo pazuri.

Msikilize Chokoraa hapo chini.

Comments