MTOTO wa nguli wa mipasho kutoka TOT Taarab, Mwanamtama Amir, Asia Mzinga, jioni hii ameingia Studio, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam kurekodi kibao kipya ndani ya kundi lake la Mashauzi Classic Modern Taarab.
Akizungumza dakika chache zilizopita, Asia alikitaja kibao hicho kuwa ni 'Wema Hauozi Ubaya Haulipizwi', ambacho ni matayarisho ya albamu yao ijayo inayokwenda kwa jina la 'Sura Surambi'.
Asia alisema kuwa, katika kibao hicho kilichopo kwenye miondoko inayochezeka, wanajamii wanaaswa kuwa na utamaduni wa kufanyiana mambo mema kwavile, ubaya haumpendezi mtu.
"Najisikia faraja leo kuingia Studio kwa sababu ni mara yangu ya kwanza tangu nianze kufanyakazi ya muziki miaka kadhaa nyuma," alisema Asia.
Comments
Post a Comment