ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN ameisawazishia Arsenal wakati Tottenham Hotspur ilipolazimisha sare ya 1-1 ugenini.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu uliochezwa Emirates Stadium, Tottenham Hotspur walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 56 kupitia kwa Chadli kalba ya Oxlade-Chamberlain kusawazisha dakika ya 74.
Arsenal ikaendelea kukumbwa na janga la majeruhi baada Mikel Arteta na Aaron Ramsey kushindwa kuedelea na mchezo baada ya kupata maumivu ya musuli.
Katika hali halisi, Arsenal walistahili kushinda hasa kwa namna Alexis Sanchez, Mesut Ozil and Santi Cazorla walivyokuwa wanaonana ukingoni mwa mchezo.
Arsenal: Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta (Flamini 28), Oxlade-Chamberlain, Ramsey (Cazorla 45), Wilshere (Sanchez 63), Ozil, Welbeck.
Tottenham Hotspur: Lloris, Naughton, Kaboul, Vertonghen, Rose (Dier 83), Mason, Capoue, Lamela, Eriksen (Lennon 62), Chadli (Bentaleb 80), Adebayor.
Comments
Post a Comment