ARSENAL KAMA HOMA YA VIPINDI …YANG’OLEWA NA SOUTHAMTON KOMBE LA LIGI … Kipa mpya David Ospina atunguliwa bao la mita 30
JUMAMOSI iliyopita Arsenal ilitandaza soka la hali ya juu katika mechi ya Barclays Premier League ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Aston Villa, lakini Jumanne usiku mambo yakawa kinyume kwenye mpambano wa Capital One Cup ulioushuhudia Washika bunduki hao wakitupwa nje na Southampton kwa bao 2-1.
Katika mchezo wao wa Jumamosi, Arsenal ikajivunjia rekodi yao ya miaka miwili ilioyopita ya kutandaza pasi nyingi, ambapo ilipiga jumla ya pasi 741, lakini kwa Southampton ngoma ikawa ngumu.
Arsenal wakaongoza kwa bao la bonge ya free-kick iliyopigwa na Alexis Sanchez katika dakika ya 14, bao ambalo lilidumu kwa dakika sita tu baada ya Dusan Tadic kusawazisha kwa penalti iliyokuja kufuatia rafu ya Tomas Rosicky kwa Sadio Mane.
Vijana wa Arsenal Wenger wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wakadhidhirisha kuwa wao ni kama homa ya vipini – leo wazuri, kesho wabaya – baada ya Nathaniel Clyne kufunga kwa bao la aina yake la mita 30.
Hiyo ilikuwa dakika ya 40 ambapo kipa mpya wa Arsenal David Ospina aliyekuwa akicheza mechi yake ya kwanza akashuhudia akitunguliwa kwa bao la mbali lililoing'oa timu yake kwenye michuano ya Capital One.
Kiungo wa Arsenal Abou Diaby akaanza mchezo wake wa kwanza katika mechi za kimashindano tangu mwezi Machi 2013 alipoumia kwenye mchezo wa Capital One
Arsenal: Ospina 4; Bellerin 5 (Akpom 86), Chambers 6.5, Hayden 5, Coquelin 5; Rosicky 5, Diaby 5.5 (Cazorla 67); Campbell 5.5 (Oxlade-Chamberlain 71), Wilshere 5, Podolski 4; Sanchez 6.
Southampton: Forster 6; Clyne 8, Fonte 7, Gardos 7.5, Targett 7 (Bertrand 85); Wanyama 6.5, Schneiderlin 9; Mane 7.5 (Long 72), Davis 7, Tadic 7.5; Pelle 7.
Comments
Post a Comment