Meneja Mkuu wa SSB, Sheikh                Said Muhammad (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Sh.                milioni 10 kwa Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (kulia).                Wanaoshuhudia ni viongozi wengine wa TASWA kutoka kushoto                Shijja Richard (Mweka Hazina), Amir Mhando (Katibu Mkuu)                na Egbert Mkoko (Makamu Mwenyekiti). 
            KAMPUNI ya Said Salim                Bakhresa Group Limited, leo imetoa kiasi cha Sh. Milioni                10 kwa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania                (TASWA) kwa ajili ya tuzo za Wanamichezo Bora nchini,                zilizopangwa kufanyika Desemba 12, mwaka huu.
            Akikabidhi fedha hizo,                Meneja Mkuu wa SSB Limited, Sheikh Said Muhammad Said                katika ukumbi wa City Sports Lounge, Mtaa wa Samora, Dar                es Salaam, amesema kwamba wanatoa mchango huo ili                kuwezesha zoezi hilo lifanikiwe. 
            "Kwanza nasema naomba                nitoe shukrani zangu za dhati kwa niaba ya kampuni kwa                TASWA kutufuata kutuomba tuchangie tuzo hizi. Sisi tupo                mstari wa mbele katika kuunga mkono harakati zote za                kimaendelea katika sekta ya michezo nchini,"amesema.Sheikh                Said amesema kwamba SSB inajivunia kuwa sehemu ya shughuli                hiyo na inawatakia kila la heri TASWA ili wafanikishe                mchakato huo.
            Kwa upande wake,                Mwenyekiti wa TASWA, Juma Abbas Pinto amesema kwamba                wanashukuru kwa mchango huo wa SSB, ambao unafungua mfuko                wa fedha za kuendehea zoezi hilo unaohitaji Sh. Milioni                120.
            "Tumejiwekea utaratibu                kwamba baada ya kufanya mazungumzo na watu mbalimbali na                kutukubalia kutusaidia zoezi hili, tutakuwa tunawatangaza                mmoja baada ya mwingine na kiwango wanachotoa,".
            "Kwa leo tunaanza na SSB,                lakini tutarajie kama si Jumapili basi Jumatatu tutakutana                tena hapa hapa kwa ajili ya kumtangaza mdhamini mwingine,"                amesema Pinto. 
            Katibu wa TASWA, Amir                Mhando kwa upande wake amesema maandalizi yanaendelea                vizuri na ameomba ushirikiano wa kutosha baina ya                Waandishi wa Habari nchini, ili zoezi hilo lifane. 
            Tuzo za wanamichezo Bora                nchini, mwaka jana zilishindwa kufanyika baada ya                waliokuwa wadhamini wake, Kampuni ya Bia ya Serengeti                (SBL) kujitoa dakika za mwishon
           
Comments
Post a Comment