XABI ALONSO ATANGAZA KUSTAAFU TIMU YA TAIFA HISPANIA


XABI ALONSO ATANGAZA KUSTAAFU TIMU YA TAIFA HISPANIA

Kiungo nyota wa Real Madrid, Xabi Alonso ameamua kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Hispania.Alonso amevunja ukimya na kutangaza kustaafu akiwa katika hatua za mwisho kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani kwa kitita cha pauni milioni 5.
Kiungo huyo mkabaji mwenye miaka 33, atajiunga na Bayern badala ya Sami Khedira ambaye alikuwa anawaniwa na Arsenal na mabingwa hao wa Ujerumani.
Madrid wameamua kumbakiza na kumuachia Alonso ambaye analazimika kukaa benchi kutokana na kutua kwa Toni Kroos akitokea Bayern.


Comments