WENGER ASEMA HAJUTII KUTOMSAJILI TENA FABREGAS


WENGER ASEMA HAJUTII KUTOMSAJILI TENA FABREGAS

On song: Cesc Fabregas impressed on his Premier                    League return for Chelsea at Burnley

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa hajutii hata kiduchu kutomsajili tena kiungo Cesc Fabregas licha ya nyota huyo wa Hispania kung'ara kwenye mechi ya Chelsea na Burnley.

Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal, ameibukia Stamford Bridge kiangazi hiki akitokea Barcelona na akakisaidia kikosi cha Jose Mourinho kuichabanga Burnley 3-1.

Lakini Wenger akasisitiza kuwa hajutii uamuzi wake kutomrejesha Fabregas Arsenal.

Wenger amesema: "Sijutii kwa Fabregas kujiunga Chelsea. Kitu pekee ninachojilaumu ni pale alipoondoka hapa.

"Ni maajabu kumuona Fabregas kwenye jezi ya Chelsea. Lakini tunapaswa kukubali. Ilikuwa ngumu kwangu kumuona akiondoka lakini tukakubali kuwa ameondoka." 



Comments