WAKALA WA VIDAL ATUA ENGLAND KUMALIZANA NA MANCHESTER UNITED …Juventus waanza kusaka kiungo mbadala, Arsenal kuwa mwathirika wa kwanza
WAKALA wa Arturo Vidal - Fernando Felicevich jana alikuwa jijini Manchester katika kile kinachoaminika ni kukamilisha mpango wa kiungo huyo wa Juventus kuhamia Manchester United kabla dirisha la usajili halijafungwa.
Fernando Felicevich ambaye pia ni wakala wa Alexis Sanchez aliyesajiliwa na Arsenal kutoka Barcelona, anatajwa kama mtu asiyeshindwa jambo linapokuja suala la uhamisho wa mchezaji wake.
Ripoti kutoka Hispania zinasema Manchester United na Juventus wako katika mazungumzo mazito ya kujadili bei ya Vidal.
Tayari inasemwa kuwa Juventus wameanza mipango ya kumsajili Adrien Rabiot kama mbadala wa Vidal. Rabiot kinda wa Ufaransa anawaniwa pia na Arsenal.
Rabiot aliyeanza kuichezea PSG miaka miwili iliyopita akiwa na umri wa miaka 17, alionekana yuko njiani kutua Arsenal lakini ujio wa Juventus unaweza ukabadili mwelekeo wa kiungo huyo.
Hii inataoa picha moja – Kama Vidal atatua United, basi Arsenal inaweza kuwa mwathirika wa kwanza wa usajili huo endapo Juventus itafanikiwa kumsajili Rabiot aliyekuwa akiwaniwa kwa udi na uvumba na Arsene Wenger.
Comments
Post a Comment