Van Gaal: Huenda ikatuchukua Mwaka Mzima Kuepuka Madhila Haya ya Aibu Kwa Team ya Man United


Van Gaal: Huenda ikatuchukua Mwaka Mzima Kuepuka Madhila Haya ya Aibu Kwa Team ya Man United
Meneja wa klabu ya Man Utd Aloysius Paulus Maria van Gaal amelia na kikosi chake ambacho usiku wa kuamkia hii leo kiliendelea kula msoto wa kutopata matokeo mazuri tangu msimu wa soka huko nchini Uinmgereza ulipoanza August 16.

van Gaal amesema kikosi chake hakikucheza vizuri wakati wa mchezo wa michuano ya kombe la ligi dhidi ya klabu ya Milton Keynes Dons ambao waliibuka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri na kuwatupa nje ya michuano hiyo mashetani wekundu.

van Gaal amesema makosa ya kipuuzi yaliyofanywa na wachezaji wake hususan waliocheza safu ya ulinzi yalikuwa chagio kubwa kwa wapinzani wao kupata mabao kwa urahisi, hivyo hana budi kuwasilisha lawama zake kwa wachezaji aliokuwa amewapa jukumu la kucheza hapo jana.

Wakati huo huo van Gaal amesema bado anaendelea na falasafa yake ya kutengeneza mazingira mapya ya kikosi na anaamini mpango huo utafanikiwa licha ya kupita kwenye mazingira magumu katika kipindi hiki cha mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2014-15.

Amesema suala hilo linapaswa kufahamika hata kwa mashabiki wa Man Utd ambao wanahitaji kuona mafanikio yanapatikana kwa haraka haraka, lakini yeye kama meneja anatambua kipindi hiki cha mpito kinaweza kuchukua muda mrefu.

Comments