VAN GAAL ASHUSHA BOMU OLD TRAFFORD …ASEMA NI MIUJIZA MANCHESTER UNITED KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU



VAN GAAL ASHUSHA BOMU OLD TRAFFORD …ASEMA NI MIUJIZA MANCHESTER UNITED KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU

Mr Motivator: Louis van Gaal will work his magic                    at Manchester United

KOCHA wa Manchester United Louis van Gaal amesema itahijitaji miujiza kwa timu yake hiyo kuchukua taji la Ligi Kuu msimu msimu huu.

Pamoja na hayo, mdachi huyo amedai  yuko katika ari ya kufikia yale yanayoonekana hayawezekani.

Van Gaal anaamini atafikia mafanikio – na amehakikishiwa na familia ya Glazer inayomiliki timu pamoja na mtendaji wake Ed Woodward kuwa atapewa muda wa kutosha kuliko David Moyes.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Van Gaal inategemewa kuwashtua mashabiki wa United.

Van Gaal alisema: "Kushinda taji la Ligi Kuu katika msimu wa kwanza itakuwa ni maajabu.

"Simaanishi kuwa haiwezekani. Ni kitu kinachowezekana, lakini itakuwa ngumu sana.

"Natumai familia ya Glazer inaelewa hili vinginevyo nisingekubali kazi hii.

"Nilijadiliana nao kila kitu. Tulikuwa na mjadala mrefu, niko wazi kwao siku zote.

"Na hiyo ndio sababu tukajadili miaka mitatu na sio mmoja.

"Kwa uzoefu wangu wa vilabu nilivyofundisha huko nyuma, siku zote kumekuwa na mwanzo mgumu."

Van Gaal alishinda mataji katika msimu wake wa kwanza Barcelona na Bayern Munich. Unajua anasemaje kuhusu hilo? "Nadhani kocha anapaswa kuhukumiwa kwa msimu wake wa pili.

"Nilichofanya Bayern Munich ilikuwa ni miujiza kwa sababu timu haikuwa imara wakati nilipoichukua," alisema Van Gaal.



Comments