BENDI mbili zinazochukuliwa kama ndugu, Twanga Pepeta na Msondo Ngoma Jumatano hii zitafanya onyesho la pamoja kwenye ukumbi wa Annex ulioko Magomeni Mikumi jirani na ukumbi wa Lango la Jiji.
Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo, Kiroboto Juma, burudani hiyo itaanza saa 2 za usiku huku kila bendi ikijivunia nyimbo mpya kabisa.
Twanga Pepeta watakuwa na faida nyingine ya kuwa na wasanii wapya waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni ambao wanaendelea kutambulishwa katika kumbi mbali mbali huku Msondo wakijivunia hazina ya nyimbo zisizochuja.
Yote kwa yote, zinapokutana jukwaani Twanga na Msondo basi huwa ni sawa na kusema 'mtoto hatumwi dukani' – ni burudani mwanzo mwisho.
Comments
Post a Comment