TOTTENHAM YAJIANDAA KUMCHUKUA WELBECK KWA MKOPO


TOTTENHAM YAJIANDAA KUMCHUKUA WELBECK KWA MKOPO

TOTTEMHAM wanafanya jitahada za kumchukua kwa mkopo mshambuliaji Danny Welbeck wa Manchester United katika kipindi hiki ambacho Shinji Kagawa yuko njiani kwenda Borussia Dortmund.

 

Tottenham ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyommendea Welbeck ambaye anatafuta sehemu itakayomfanya awe chaguo la kwanza nje ya Old Trafford.

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino alimtazama Welbeck kwenye mechi ya United dhidi ya MK Dons katika Capital One Cup.

Ingawa United haikO tayari kuuza silaha kwa wapinzani wao, lakini inaweza kukubali dili hilo iwapo Tottenham itakubali kulipa mshahara kamili wa mshambuliaji huyo wa England pamoja na sharti la kutomtumia katika mechi dhidi yao.



Comments