FAINALI za mashindano ya                Safari Pool Taifa yajulikanayo kama "Safari National Pool                Competition 2014", mkoa wa kimichezo wa Temeke jijini Dar                es Saalaam na Dodoma zimefanikiwa kupata mabingwa wa mikoa                mwishoni mwa wiki. 
        Mkoa wa kimichezo wa                Temeke mabingwa ni klabu ya Mpo Afrika walifanikiwa                kutetea ubingwa wao wa mwaka jana wakati mkoani Dodoma                Klabu ya Delux ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa huo.
        Klabu ya Mpo Afrika na                Delux kwa kutwaa ubingwa huo zilizawadiwa pesa taslimu                Shilingi 800,000/= kila klabu pamoja na tiketi ya                kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa                kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
        Upande wa mchezaji mmoja                mmoja wanaume, Temeke; Innocent Sammy alifanikiwa kutwaa                ubingwa na Dodoma ni Rgnald Kassimu, ambao walizawadiwa                pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila mmoja katika mikoa                yao pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika                fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro kwa mchezaji mmoja                mmoja Wanaume.
        Upande wa mchezaji mmoja                mmoja Wanawaake,Temeke; Rebeca Magaigwa alitwaa ubingwa na                Dodoma ni Rehema Mussa, ambao walizawadiwa fedha taslimu                Shilingi 300,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa                yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro kwa                mchezaji mmoja mmoja upande wa Wanawake.
        Wiki hii fainali za                Safari Pool Competition 2014,ngazi ya mikoa zinatarajiwa                kuhitimishwa na mikoa ya Morogoro, Iringa na Mbeya.
        Fainali za kitaifa za                2014 za "Safari National Pool Competion" zinatarajiwa                kufanyika Septemba 14 mwaka huu, Moshi Mkoani Kilimanjaro                kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni                Tabora,Shinyanga,Dodoma                Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwan                i,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano                kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
                Meneja wa bia ya Safari                Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia) akimkabidhi kikombe                nahodha wa timu ya klabu ya mchezo wa Pool ya Mpo Afrika,                Charles Vernance mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali                za mchezo huo ujulikanao kama "Safari National Pool                Competition 2014" ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika                Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni                Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga na Kocha wa                timu ya Taifa, Denis Rungu. 
                Meneja wa bia ya Safari                Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia) akimkabidhi pesa                taslimu Shilingi 800,000/= nahodha wa timu ya klabu ya                mchezo wa Pool ya Mpo Afrika, Charles Vernance mara baada                ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo unaojulika                kama "Safari National Pool Competition 2014" ngazi ya mkoa                mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam                mwishoni mwa wiki.Kulia ni Katibu wa Chama cha Pool Taifa,                Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu. 
                Baadhi ya wachezaji wa                Pool wa klabu ya Mpo Afrika na mashabiki wakishangilia na                kikombe mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo                huo unaojulika kama "Safari National Pool Competition                2014" ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini                City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
        


Comments
Post a Comment