SIMBA SC imewafunga mabingwa wa Zanzibar, KMKM mabao          5-0 katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom          Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
        KMKM inayofundishwa na Ally Bushiri 'Bush' ambayo          Jumatano wiki hii ilifungwa 2-0 na Yanga SC, leo iligeuzwa asusa          na Wekundu wa Msimbazi.
        Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 4-0,          yaliyotiwa kimiani na Amisi Tambwe mawili, Amri Kiemba na          Shaaban Kisiga 'Malone' moja kila mmoja.
          
        Amri Kiemba ndiye aliyefungua karamu ya mabao ya            Simba SC hii leo, dakika ya tatu ya mchezo baada ya kupewa            pasi nzuri na kiungo Mrundi, Pierre Kwizera na kuwatoka            wachezaji wawili wa KMKM kabla ya kufumua shuti kali            lililogonga mwamba wa ndani wa lango.
          Amisi Tambwe akafuatia dakika            ya 14 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Salim Amour            kufuatia yeye mwenyewe kupiga mkwaju wa penalti, baada ya            kiungo, Haroun Chanongo kuangushwa kwenye boksi.
          Tambwe tena akafunga bao la            tatu dakika ya 23 akimalizia krosi maridadi ya Ramadhani            Singano 'Messi' kabla ya Kisiga kufunga la nne dakika ya 37,            kufuatia kazi nzuri ya Kiemba.
        Kipindi             ha pili, kocha Mzambia, Patrick Phiri alibadilisha kikosi            kizima akimuacha Nahodha Jopseph Owino pekee na dakika ya 60            Elias Maguri akahitimisha karamu ya mabao kwa bao safi la            tano.
          Mshambuliaji            Mganda, Emmanuel Okwi aliyetangaza juzi kurejea Simba SC            kutoka kwa mahasimu, Yanga SC usiku huu alikuwepo, lakini            alibaki benchi muda wote wa mchezo.
        |  | 
| Beki wa Simba SC, Issa Rashid 'Baba                Ubaya' akimtoka mchezaji wa KMKM | 
|  | 
| Wazito; Kutoka kulia Musley Ruwey,                Hans Poppe na Salim Abdallah 'Try Again' | 
|  | 
| Okwi katikati akiwa na Mosoti kulia na Butoyi kushoto | 
|  | 
| Amisi Tambwe na Ramadhano Singano 'Messi' kulia wakishangilia usiku huu uwanja wa Amaan | 
Comments
Post a Comment