SAMI KHEDIRA 'AISUSIA' MECHI YA REAL MADRID NA ATLETICO …AKATIMKIA UJERUMANI KUNGALIA BUNDESLIGA



SAMI KHEDIRA 'AISUSIA' MECHI YA REAL MADRID NA ATLETICO …AKATIMKIA UJERUMANI KUNGALIA BUNDESLIGA

Disgruntled: Khedira is angry that Real will not                  meet his contract demands

UVUMI wa Sami Khedira kutimka Real Madrid unazidi kupamba moto baada ya kutua Ujerumani kushuhudia mechi ya Bundesliga huku timu yake ikiwa inamenyana na Atletico Madrid kwenye Super Cup ya Hispania.

Khedira aliwasili Ujerumani Ijumaa na kupata wasaa wa kumwangalia mdogo wake Rani Khedira anayekipiga na timu ya RB Leipzig iliyokuwa ikimenyana na Aue.

Inavumishwa kuwa Sami Khedira huenda akajiunga na Bayern Munich, lakini inaaminika kuwa kiungo huyo si chaguo la kwanza la kocha Pep Guardiola, kitu ambacho kinaweza kupelekea dili hilo lisiwezekane.

Sami Khedira hakuwemo kwenye kikosi kilichapangwa kucheza na Atletico Ijumaa usiku na akaruhusiwa na kocha wake Carlo Ancelotti kwenda nje ya nchi.

Licha ya kuhusishwa na Bayern Munich, Khedira pia anatajwa pia katika uhamisho wa kwenda Manchester United na Arsenal.



Comments