LIVERPOOL imeweka mezani pauni milioni 16 kwaajili ya kupata saini ya Mario Balotelli na tayari AC Milan imeridhia mshiko huo wa wekundu wa Anfield.
Kilichobakia sasa ni makubaliano binafsi ya Liverpool na Balotelli ambaye inaaminika anataka mshahara wa pauni 125,500 kwa wiki.
Mwezi uliopita kocha Brendan Rodgers alisema Liverpool haiwezi kumsajili mchezaji huyo mtukutu wa Italia, lakini sasa anaonekana amekunjua moyo wake na kubadili mawazo.
Balotelli aliimbia Sky Italia mapema leo: "Hii itakuwa ni siku yangu ya mwisho Milanello"
Baadae akaondoka uwanja wa mazoezi Milanello akiwa ndani ya Ferrari nyekundu.
Pichani juu kabisa ni namna Balotelli atakavoonekana kwenye jezi ya Liverpool.
Comments
Post a Comment