TOM CLEVERLEY amekutana na kocha msaidizi wa Aston Villa kujadili suala la uhamisho wa kutimka Old Trafford.
Keane ambaye ni mmoja wa nyota waliojizolea mafanikio makubwa katika Manchester United, anajaribu kufanya kila awezalo kumtwaa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa kumpa ahadi ya kuwa chaguo la kwanza.
Cleverley ambaye tayari ana ofa ya pauni milioni 7 kutoka kwa Aston Villa, anawaniwa pia na Everton, Hull and Valencia.
Kiungo huyo ambaye bado hajaamua ni wapi pa kwenda, angependelea zaidi kuondoka kwa mkopo kwa msimu mmoja kabla ya kutimka bure kwenye kikosi cha Louis van Gaal kiangazi kijacho.
Comments
Post a Comment