RONALDO: NINGETUPWA JELA KAMA NINGETOA HADHARANI MAONI YANGU KUHUSU FIFA KUMPA MESSI TUZO YA KOMBE LA DUNIA


RONALDO: NINGETUPWA JELA KAMA NINGETOA HADHARANI MAONI YANGU KUHUSU FIFA KUMPA MESSI TUZO YA KOMBE LA DUNIA

Rivals: Lionel Messi and Cristiano Ronaldo will                  again go head-to-head for the La Liga title this season

SUPASTAA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema angetupwa jela kama angetoa maoni yake kuhusu FIFA kumpa tuzo ya Golden Ball mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi kwenye michuano ya kombe la dunia.

Hata hivyo Ronaldo alitoa kauli hiyo kama sehemu ya mzaha wake mara baada ya kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya.

Winner: Ronaldo kisses the Best Player in Europe                  award after beating Arjen Robben to the award

Ronaldo alikataa kuzungumza lolote juu ya nahodha wa Argentina kutajwa kama mchezaji bora wa Kombe la Dunia.

Wakati Messi akipewa tuzo hiyo baada ya kuisaidia Argentina kufika fainali ya World Cup, Ronaldo alisema anadhani nyota huyo wa Barcelona hakustahili kushinda tuzo hiyo.

Ronaldo was speaking to Portuguese TV channel TVI                  when he joked about Messi's Golden Ball win 

Akizungumza na kituo cha televisheni TVI cha Ureno, Ronaldo akatania kuhusu Messi: "Kama ningesema kila nilichokuwa nakifikiria, nadhani saa hizi ningekuwa jela," alisema Ronaldo kabla ya kucheka akionyesha kuwa anafanya mzaha.

"Kila mtu anaweza kuona na kutoa maamuzi yake, watu wa ulimwengu wa soka wana akili sana," alisema Ronaldo baada ya kuulizwa kuhusu tuzo ya FIFA kwa Messi.

"Lingekuwa swali muhimu zaidi kwake. Siwezi kutenda haki kuhusu hilo.

"Kila mmoja anafanya kazi yake, kila mmoja anafanya vizuri. Wote tunataka kuwa bora. Binafsi ndani ya akili yangu, naamini mimi ni bora." 



Comments