| Ronaldo                            akimkabidhi tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa                            Dunia, Rais wa Real Madrid, PerezMRENO Cristiano Ronaldo                            ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya                            msimu wa 2013-2014 katika sherehe                            zilizofanyika jioni ya leo mjini Monaco,                            Ufaransa.Nyota huyo wa Real                            Madrid amewapiku nyota wa Bayern Munich, kipa                            Mjerumani Manuel Neuer na winga Mholanzi,                            Arjen Robben alioingia nao fainali.  Wakati                            Neuer alishinda taji la Bundesliga na Kombe la                            Dunia msimu uliopita,                            Robben alifunga mabao 22 kwa klabu na timu                            yake ya taifa msimu uliopita na Ronaldo                            alifunga mabao 56 na kutoa pasi 15 za mabao                            Real Madrid na Ureno. Mshindi wa mwaka jana,                            Mfaransa Franck Ribery hakuingia fainali. | 
                
Comments
Post a Comment