Marcos Rojo amapata kibali cha kufanya kazi nchini England na ilitegemewa jumamosi hii aanze kuitumikia United lakini taarifa kutoka UK zinasema kwamba mchezaji huyo wa kiargentina anaweza bado asipate ruhusa ya kuichezea klabu mpya kutokana na ugomvi wa kisheria uliopo kati ya Sporting Lisbon na kampuni ya Doyen Sports iliyokuwa inamiliki haki zake za usajili kwa asilimia 75.
United imemsajili Rojo kutoka Lisbon kwa ada ya jumla ya £16m lakini wamelipa £8m kwa sasa na baada watalipa £4m X2. Premier League hairuhusu suala la 'umiliki wa pande 3' (Third Part Ownership) - mtindo ambao unaruhusiwa kwenye nchi kama Ureno alipotoka Rojo. Tatizo la Third Part Ownership liliwahi kuiletea matatizo West Ham huko nyuma waliposajili Carlos Tevez na Javier Alejandro Mascherano
Comments
Post a Comment