ROJO AENDA MADRID, KUHANGAIKIA VISA



ROJO AENDA MADRID, KUHANGAIKIA VISA
Beki Marcos Rojo amelazimika kupanda ndege na kurejea jijini Madrid, Hispania akilazimika kusubiri kupatikana kwa visa na kibali cha kazi ili arejee kujiunga na timu yake mpya ya Manchester United.Imeelezwa akiwa Madrid, Rojo raia wa Argentina atafanyiwa mahojiano yatakayomuwezesha kupata visa hiyo.Ingawa kumekuwa na ugumu unaotokana na suala la kesi yake inayomkabili iliyotokea miaka mitano iliyopita baada ya kuzozana na majirani zake.
Kwa sheria kali za England, inatakiwa kuwa na uhakika kuwa Rojo hatawasumbua majirani zake atakaoishi nao jijini Manchester na ikigundulika alikuwa mkorofi, basi anaweza kunyimwa viza na United ikamkosa.
Hata hivyo, wakati Rojo akiwa Madrid, uongozi wa Man United umesisitiza suala hilo linakwenda ukingoni na beki huyo iliyemsainisha kwa pauni milioni 16 kutoka
Sporting Lisbon ya Ureno, ataungana na wenzake na kuanza kazi.


Comments