REAL MADRID YATHIBITISHA KUMUUZA XABI ALONSO KWA BAYERN MUNICH


REAL MADRID YATHIBITISHA KUMUUZA XABI ALONSO KWA BAYERN MUNICH
REAL MADRID YATHIBITISHA KUMUUZA XABI ALONSO KWA BAYERN            MUNICH

XABI Alonso amekamilisha usajili wa pauni milioni 5 kwenda Bayern Munich akitokea Real Madrid.

Real Madrid imetangaza kupitia mtandao wao rasmi kuwa: "Real Madrid na Bayern Munich zimefikia makubaliano ya dili la uhamisho wa Xabi Alonso.

Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool alikuwa akihusishwa na Manchester United baada ya miaka yake mitano Bernabeu, lakini sasa anajumuika na kocha Mhispania Pep Guardiola.

Alonso mwenye umri wa miaka 32 anakwenda Bayern katika kipindi ambacho timu hiyo ina balaa la majeruhi la viungo wake Javi Martinez, Bastian Schweinsteiger na Thiago Alcantara.

Mkuu wa mambo ya fedha wa Bayern Munich Jan-Christian Dreesen sambamba na Matthias Sammer, wameviambia vyombo vya habari Alhamisi kuwa kimsingi wamefikia makubaliano na kuthibitisha hayo, mchezaji huyo aliwasili jioni ya Alhamisi kufanya vipimo vya afya.

Confirmation: Xabi Alonso has joined Bayern Munich                  from Real Madrid in a £5m deal

Usajili wa Alonso ambo unakuwa ni wa tano kwa wachezaji wa Kihispania kwenda Bayern wakiwemo Pepe Reina, Juan Bernat, Thiago Alcantara na Martinez, unakuja siku moja tu baada ya usajili wa beki Benatia kutoka AS Roma.



Comments