CRISTIANO RONALDO amefunga goli namba 255 katika mchezo wake wa 250 kwa Real Madrid wakati timu yake ilipopata ushindi wa mbinde wa 2-0 kwa timu iliyopanda daraja Cordoba.
Katika mchezo huo wa La Liga, Ronaldo alifunga bao lake katika dakika ya 90, baada ya Karim Benzema kufunga goli la kwanza dakika ya 30.
Kumuuza Angel Di Maria, kipigo dhidi ya Atletico Madrid kwenye Spanish Super Cup, kushindwa kumsajili Radamel Falcao ni vitu vinavyoongeza presha kwa mabingwa hao wa Ulaya hasa kwa namna walivyobanwa na Cordoba.
Wangeweza kujikuta wakiwa 1-1 kama goli la mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Xisco lisingekataliwa kwa madai ya kuotea.
Real Madrid: Casillas, Arbeloa, Ramos, Pepe, Marcelo, Kroos, Modric, Bale, James, Ronaldo, Benzema.
Cordoba: Carlos; Gunino, Inigo, Pantic, Crespo, Rossi, Garai, Pinillos, Ryder, Lopez Silva, Havenaar.
Comments
Post a Comment