PAUL SCHOLES AHOJI USAJILI WA DALEY BLIND MANCHESTER UNITED …asema United inahitaji wachezaji halisi wa kiungo



PAUL SCHOLES AHOJI USAJILI WA DALEY BLIND MANCHESTER UNITED …asema United inahitaji wachezaji halisi wa kiungo

daley blind, manchester united, man united, man                    utd, louis van gaal, van gaal, lvg, mufc, premier                    league, epl, bpl, world cup, holland, paul scholes,

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, PAUL SCHOLES amehoji kuhusu timu hiyo kumsajili beki wa Ajax Daley Blind.

Blind (pichani juu) anatarajiwa kutua Old Trafford kwa ada ya pauni milioni 17.5 ambapo timu zote mbili (Ajax na United) zimethibisha kukubalina dili la nyota huyo wa kimataifa wa Holland.

Daley Blind mwenye umri wa miaka 24 aling'ara kwenye kombe la dunia huko Brazil chini kocha Louis van Gaal ambapo alitumika zaidi kama beki wa kushoto anayepanda (left wing-back).

Scholes anaamini ukiraka wa Blind unaweza ukamfanya atumike zaidi kama kiungo mkabaji.

"Sina uhakika atacheza katika nafasi gani," anasema Scholes huku akionyesha shaka iwapo mchezaji huyo atahimili nafasi ya beki wa kushoto kwenye ligi yenye mikikimikiki kama ya England.

"Sidhani kama ana nguvu za kutosha kucheza kama beki tatu England.

"Sehemu pekee anayoweza kucheza hapa ni kiungo mkabali, lakini je ni jibu? Ndiye suluhisho la eneo hilo? Ni jambo la kusubiri.

"Hatujui ni nafasi gani atakayocheza. United kwa sasa haitakiwi kubahatisha. Wanahitaji wachezaji halisi wa kiungo cha kati.

Blind ni mchezaji mzuri lakini kwa kiungo? Sijui!"



Comments