OLIVIER GIROUD NJE HADI 2015, ARSENAL YAHAHA NA WELBECK … United yadhamiria kulipa kisasi cha kunyimwa Vermaelen


OLIVIER GIROUD NJE HADI 2015, ARSENAL YAHAHA NA WELBECK … United yadhamiria kulipa kisasi cha kunyimwa Vermaelen

Target: Arsenal are set to make a bid for                  Manchester United's out of favour forward Danny Welbeck

ARSENAL hali ni tete sasa baada kubainika kuwa mshambuliaji wake Olivier Giroud anaweza kuwa nje ya dimba kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyodhaniwa hapo mwanzo.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa akakaa nje ya mwanja hadi mwaka 2015 kufuatia kuumia kwake kiwiko cha mguu.

Crocked: Arsenal need to replace Giroud, with the                  striker set to be out for more than three months

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger sasa anapiga hesabu za kupata saini ya mshambuliaji wa Manchester United Danny Welbeck lakini inaaminika Mashetani Wekundu wamedhamiria kuinyima Arsenal mchezaji huyo kama sehemu ya kulipa kisasi na kunyimwa beki Thomas Vermaelen aliyeuzwa Barcelona.

Giroud, ambaye alipata maumivu ukingoni mwa mchezo wa Ligi Kuuu ulioisha kwa sare ya 2-2 dhidi ya Everton, alionekana kama ataweza kucheza mechi ya kufa na kupona ya mchujo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Besiktas.

Danny Welbeck alianza katika mechi ya Capital One Cup Jumanne usiku ambayo Manchester United ilibugizwa bao 4-0 na MK Dons, lakini hakuanza hata mchezo mmoja wa Ligi Kuu.



Comments