NEEMA ZAZIDI KUMDONDOKEA ROONEY …ACHAGULIWA KUWA NAHODHA MPYA WA ENGLAND


NEEMA ZAZIDI KUMDONDOKEA ROONEY …ACHAGULIWA KUWA NAHODHA MPYA WA ENGLAND

Moving forward: Wayne Rooney has been handed the                    England captaincy by manager Roy Hodgson 

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney amezidi 'kutakata' baada ya kutajwa rasmi kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya England.

Wiki chache nyuma, Rooney alipewa unahodha wa Manchester United na sasa neema nyingine imemdondokea.

Nyota huyo wa miaka 28 anachukua nafasi ya Steven Gerrard aliyetangaza kuachana na soka la kimataifa baada ya kampeni mbovu za England kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.

Lampard aliyekuwa nahodha msaidizi, nae pia alitangaza kuachana na soka la kimataifa mapema wiki hii.



Comments