MWIMBAJI mahiri wa Mashujaa Band, Pasyaa Budanzi (pichani juu) amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na mama yake mzazi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mashujaa Group inayomiliki Mashujaa Band, Mamaa Sakina ameiambia Saluti5 kuwa mama mzazi wa Pasyaa amefari juzi nchini Congo DRC.
Mamaa Sakina amesema mwimbaji huyo yuko njiani kurejea Dar es Salaam ili aweze kwenda Congo kwenye mazishi ya mama yake.
Pasyaa alikuwa mikoani kwenye ziara ndefu ya Mashujaa Band.
Saluti5 inampa pole nyingi Pasyaa.
Comments
Post a Comment