Mashindano ya FEASSSA yaanza kutimua vumbi


Mashindano ya FEASSSA yaanza kutimua vumbi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe akitoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA (Federation of East Africa Secondary Schools Sports Association), jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) Mhe. Hawa Ghasia akiwakaribisha wanamichezo kutoka Afrika Mashariki katika mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 1 septemba mwaka huu 2014.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (wakwanza kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (kulia) wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yyakiendelea wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Maandalizi ya FEASSSA Bi.Mwantumu Mahiza akielezea jinsi Tanzania ilivyojiandaa kufanikisha mashindano hayo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar esSalaam.
Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Shule ya Sekondari Makongo Tanzania katika picha ya pamoja kabla ya mechi na Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Uganda wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule za Sekondari kutoka Tanzania ambao wanashiriki mashindano ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki wakiwa kwenye maandamano ya uzinduzi wa mashindano hayo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.


Comments