BEKI mpya wa Manchester United Marcos Rojo hataruhusiwa kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya MK Dons Jumanne usiku kwa vile kibali chake cha kufanya kazi England bado hakijakamilika.
Louis van Gaal alitegemea beki huyo angecheza katika mchezo wa 1-1 dhidi ya Sunderland Jumapili, lakini sasa anaamini atampata Jumamosi ijayo wakati United itakapomenyana na Burnley kweye mchezo wa Ligi Kuu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 aliyesajiliwa kwa pauni milioni 16 kutoka Sporting Lisbon, hataruhisiwa kucheza hadi kibali cheke kikamilike.
Kukosekana kwa Rojo kunaongeza msururu mrefu wa wachezaji wanaokosekana kwenye kikosi cha United wakiwemo Luke Shaw, Michael Carrick, Marouane Fellaini, Jesse Lingard, Rafael da Silva na Ander Herrera ambao wote ni majeruhi.
Van Gaal anategemewa kuendelea kuwapa nafasi wachezaji chipukizi kama Michael Keane na Tyler Blackett kwenye mchezo wa Jumanne usiku.
Comments
Post a Comment