MAPACHA WATATU KUFANYA BONANZA KUBWA ILALA JUMAPILI HII …Mgeni wa heshima Mh Mussa Azzan Zungu

MAPACHA WATATU KUFANYA BONANZA KUBWA ILALA JUMAPILI HII …Mgeni wa heshima Mh Mussa Azzan Zungu
MAPACHA WATATU KUFANYA BONANZA KUBWA ILALA JUMAPILI HII            …Mgeni wa heshima Mh Mussa Azzan Zungu

JUMAPILI hii tarehe 24 August, kutakuwa na bonanza kubwa la aina yake Ilala litakalohusisha michuano ya soka pamoja na burudani ya nguvu kutoka kwa bendi ya Mapacha Watatu "Wakali wa Town".

Bonanza hilo litakaloanza asubuhi hadi usiku, litafanyika katika viwanja vya Garden Ilala ambapo kwa mujibu wa meneja wa Mapacha Watatu, Hamis Dacota, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa Ilala Mheshiwa Mussa Azzan Zungu.

Dacota ameiambia Saluti5 kuwa bonanza hilo limeandaliwa na Vicky Dong King ikiwa ni maalum kwaajili ya kuwatutanisha pamoja wana wa Ilala.

Mapacha Watatu kwasasa wanafanya vizuri wakiwa na wimbo wao mpya "Sauti ya Marehemu" utunzi wake Jose Mara.

Comments