MANCHESTER UNITED YAENDELEA KUSAKA USHINDI WA KWANZA BILA MAFANIKIO, DI MARIA ALETA MATUMAINI …MAN CITY NAYO YACHUKUA KICHAPO


MANCHESTER UNITED YAENDELEA KUSAKA USHINDI WA KWANZA BILA MAFANIKIO, DI MARIA ALETA MATUMAINI …MAN CITY NAYO YACHUKUA KICHAPO

Closely monitored: Di Maria (centre) tries to                    fend the ball from Burnley opponents

MANCHESTER UNITED imecheza mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu na kubanwa sare ya 0-0 na Burnley.

Ikimchezesha mshambuliaji wake mpya Angel Di Maria, United ikajikuta  inakutana na kigingi wakati ikisaka ushindi wake wa kwanza.

Hadi sasa kikosi cha Louis van Gaal kimefungwa mechi moja na kupata sare 2 hali inayowafanya waninginie kwenye nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu.

Hata hivyo Di Maria aliyenunuliwa kwa pauni milioni  60 alingara sana na kulazimisha wachezaji wa Burnley watumie zaidi mbinu za kumkata viatu ili kumdhibiti na ilibidi Van Gaal ampumzishe ilipotimu dakika ya 69 na nafasi yake kuchukuliwa na Anderson.

Wakati United ikipata sare, watani zao Manchester City wakapa kipigo cha kwanza baada ya kunyukwa 1-0 na Stoke City.

Bao la Stoke City liliwekwa kimiani na mchezaji wa zamani wa United Mame Biram Diouf kunako dakika ya 58.



Comments