MANCHESTER UNITED YAAMBULIA POINTI YA KWANZA, YABANWA NA SUNDERLAND …safu ya kiungo bado yamtesa Van Gaal


MANCHESTER UNITED YAAMBULIA POINTI YA KWANZA, YABANWA NA SUNDERLAND …safu ya kiungo bado yamtesa Van Gaal
MANCHESTER UNITED YAAMBULIA POINTI YA KWANZA, YABANWA NA            SUNDERLAND …safu ya kiungo bado yamtesa Van Gaal

HALI bado tete kwa Manchester United ambapo ushindi umekuwa ni kitu adimu kwao baada ya kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Sunderland.

United iliyofungwa 2-1 na Swansea katika mchezo wao wa kwanza, ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 17 kupitia kwa Juan Mata.

Lakini Sunderland waliokuwa nyumbani, wakachomoa dakika ya 30 kwa bao lililowekwa kimiani na mchezaji wao mpya Jack Rodwell.

Kocha wa United, Van Gaal aliyeendelea kutumia mfumo wa 3-5-2 aliteswa kwa kukosekana kwa safu nzuri ya kiungo iliyoshindwa kuunganisha timu hali iliyofanya United itegemee zaidi mashambulizi kupitia kwa mabeki wake wanaopanda Ashley Yong na Antonio Valencia.

Katika mechi zingine, Tottenham iliichapa QPR 4-0 kwa mabao yaliyofungwa na Nacer Chadl aliyefunga mara mbili, Eric Dier na Emmanuel Adebayor. Hull City ikatoka sare ya 1-1 na Stoke City.

Sunderland: Mannone 6.5, Vergini 8.5, O'Shea 6.5, Brown 7, Van Aanholt 5.5, Larsson 6, Cattermole 8, Rodwell 6.5 (Gomez 63, 6), Buckley 7.5 (Bridcutt 79), Fletcher 6.5 (Altidore 76, 6), Wickham 7. 

Manchester United: De Gea 6, Jones 5, Smalling 5.5 (Michael Keane 44, 5.5), Blackett 5, Valencia 6.5, Fletcher 5 (Januzaj 64, 6), Cleverley 5.5, Young 4.5, Mata 5.5, Van Persie 5.5 (Welbeck 64, 5), Rooney 6. 



Comments