MANCHESTER UNITED MAHARAGE YA MBEYA, YAPIGWA 4-0 NA TIMU YA DARAJA LA KWANZA ...yatolewa Capital One Cup
MAMBO yameanza kumwendea kombo kocha mpya wa Manchseter United Louis van Gaal baada ya timu yake kupigwa 4-0 na kutolewa kwenye michuano ya Capital One Cup.
Akiwa anasaka ushindi wake wa kwanza kwenye mechi za kimashindano, Van Gaal akajikuta akishuhudia timu yake ikifungwa kama imesimama na timu ya daraja la kwanza MK Dons.
Will Grigg alikuwa mwiba kwa United baada ya kufunga mabao mawili katika dakika ya 25 na 63 huku mtu aliyeingia kuchukua nafasi ya kipindi cha pili Benik Afobe nae pia akikwamisha mipira wavuni mara mbili dakika ya 70 na 84.
Sentahafu wa United Johnny Evans ambaye ndio kwanza anarejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi, alihusika vilivyo na bao la kwanza baada kuvurunda na kumpasia mpira Will Grigg.
MK Dons: Martin, Baldock, Kay, McFadzean, Lewington, Carruthers, Potter, Reeves, Alli, Bowditch, Grigg.
Subs: Green, Spence, Randall, McLoughlin, Powell, Hitchcock, Afobe.
Man Utd: De Gea, Vermijl, Evans, Michael Keane, James, Janko, Anderson, Kagawa, Powell, Welbeck, Hernandez.
Subs: Januzaj, Zaha, Amos, Wilson, Pereira, McNair, Thorpe.
Comments
Post a Comment