MANCHESTER UNITED KUMSAJILI BEKI KITASA DALEY BLIND WA AJAX

Mchezaji nyota wa kimataifa wa Holland na Ajax, Daley Blind.
MANCHESTER UNITED imekubali kulipa dau la pauni milioni 14.2 iliyohitajiwa na Ajax ili kumsajili nyota wa kimataifa wa Holland Daley Blind.Kilichobakia sasa kwa Blind mwenye umri wa miaka 24 ni kukubaliana na United kuhusu maslahi yake binafsi na kwenda kufanya vipimo vya afya.United inaamini mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto, beki wa kati na kiungo mkabaji, atakamilisha usajili wake kabla dirisha la usajil halijafungwa.

Habari kutoka Holland zinasema ada iliyofikiwa ni pauni 14.2 ambapo United ikathibitisha kupitia akaunti yake ya Twitter kuwa wamekubaliana na ada hiyo na watatangaza kitakachojiri hapo baadae.

Comments